Martha Mwaipaja – Asante Yesu

Martha Mwaipaja – Asante Yesu Mp3 download

Martha Mwaipaja Asante Yesu Mp3

Martha Mwaipaja Asante Yesu Mp3 Download Fakaza Gospel. Veteran Tanzanian gospel singer, Martha Mwaipaja comes through with a brand new song which is titled Asante Yesu.

Martha Mwaipaja Mp3 Download. Listen online, and enjoy The Lyrics, Video of your favorite Music

Stream, Listen, and Download Below.

DOWNLOAD MP3 Martha Mwaipaja – Asante Yesu

Asante Yesu Lyrics By Martha Mwaipaja

Asante bwana yesu kwa wema wako ulijitoa kwaajili yetu kama usingelikuwa wewe maisha yetu yangelikuwaje
Asante bwana yesu kwa wema wako ulijitoa kwaajili yetu kama usingelikuwa wewe maisha yetu yangelikuwaje
Wewe umetangaza pumziko la kweli kwamba wote wenye mizigo waitue kwako kama sio wewe mwokozi kutupumzisha mizigo yetu tungeitua wapi
Tena umetanga kwa wenye magonjwa kwamba kwa kupigwa kwako wote wamepona kama usingejitoa kupigwa mtini wenye magonjwa wangeponywa na nani
Tena umesema na wote wenye kilio kwamba siku moja watanyamazishwa kama usingeyaona machozi ya wengi nani angeweza kujinyamazisha mwenyewe(Asante)
Asante bwana yesu kwa wema wako ulijitoa kwaajili yetu kama usingelikuwa wewe maisha yetu yangelikuwaje
Asante bwana yesu kwa wema wako ulijitoa kwaajili yetu kama usingelikuwa wewe maisha yetu yangelikuwaje
Hata kwa walioshushwa chini wewe upo unamwinua mnyonge kutoka chini
Unakichagua kionekacho dhaifu ili upate kukiabisha chenye nguvu
Hata katika shida tunazopitia umesema yesu hautotuacha maana mkono wako si mfupi hata usiweze kututoa kwenye tabu
Ni kweli tunapita kwenye misukosuko lakini tunajua yesu wetu upo nasi maana umesema ni heri wenye huzuni siku yao ipo watafarijika
Asante bwana yesu kwa wema wako ulijitoa kwaajili yetu kama usingelikuwa wewe maisha yetu yangelikuwaje
Asante bwana yesu kwa wema wako ulijitoa kwaajili yetu kama usingelikuwa wewe maisha yetu yangelikuwaje
Hata kwa wasio na baba wewe upo umesema nikuite baba kama usingeuona ukiwa wangu ni nani leo ningemwita baba
Hata kwa mama yangu nimekuona umemvusha katika ujane wa tabu kwa misukosuko mingi aliyopitia bila wewe yesu asingeliweza
Wewe ni mungu utabaki kuwa mungu unatuwazia mawazo yaliyo mema ungekuwa mwingi wa ghadhabu kwa wanadamu ni nani leo hii angesimama
Asante bwana yesu kwa wema wako ulijitoa kwaajili yetu kama usingelikuwa wewe maisha yetu yangelikuwaje
Asante bwana yesu kwa wema wako ulijitoa kwaajili yetu kama usingelikuwa wewe maisha yetu yangelikuwaje
Bonus
Kuna wakati wa kulia wakati wa kuombeleza wakati wa kusema mungu wangu mbona umeniacha
Maana hakuna wakati mgumu kama wakati wa shida hata ndugu yako wa damu atajitenga nawe
Utasema labda mpendwa mwenzangu atanisaidia hata mpendwa mwenzio atajitenga nawe
Utasema labda mpendwa mwenzangu atanisaidia hata mpendwa mwenzio atajitenga nawe
Nimejifunza kwamba wakati wa matatizo hata yule aliyekupenda anajitenga nawe maana hata wakati wa yesu…