Rose Muhando Namtaka Yesu Mp3
Rose Muhando Namtaka Yesu Mp3 Download Fakaza Gospel. The Gospel music artist, Rose Muhando comes through with a new song tagged “Namtaka Yesu”.
Rose Muhando Mp3 Download. Listen online, and enjoy The Lyrics, Video of your favorite Music
Stream, Listen, and Download Below.
DOWNLOAD MP3: Rose Muhando – Namtaka Yesu
Lyrics: Namtaka Yesu
Yahwéh!
Nainua macho nitazame pande zote Nione kama yupo wa kumweleza shida zangu Naona hakuna wote wamepungukiwa Hawana furaha, hawana matumaini Nakumbuka habari za yule mwanamke Aliyetokwa damu miaka kumi na miwili Aliposikia kwamba Yesu anapita, aliazimia akasema moyoni mwake Nitajisogeza mpaka nifike kwa Yesu, nitajisogeza mbele ya umati wa watu Nitajipenyeza mpaka nifike kwa Yesu, niguse pindo lake ili nipate uzima Akajisogeza mpaka kafika kwa Yesu, akagusa pindo lake mara akawa mzima, akaponaNami Bwana ni sawa na yule mwanamke, aliyetokwa damu miaka kumi na miwili
Nimeshasikia habari za matendo yako Nimeazimia nami Bwana moyoni mwangu, nitahakikisha mpaka nifike kwako Yesu Niguse pindo lako kansa iniondokee Niguse pindo lako umasikini ukae mbali nami Nimechoka kuonewa mimi namtaka Yesu Nasema sikubali kufa na magonjwa yangu Nitajisogeza mpaka nifike kwa Yesu, niponeKuna watu wengine jamani wananishangaza
Unapowaambia habari za kumwona Yesu Wanaanza kuuliza eti unatoka wapi Wananisahangaza na maswali ya ajabu Unatokea wapi, kanisa lako ni lipi? Nasema nipisheni, mimi namtaka YesuMaswali sitaki, mimi namtaka Yesu
Nimweleze shida zangu ili nipate kupona Nimweleze shida zangu ili nipate amani Nisikie furaha nipate kuburudika moyoniKwa habari ya dhambi huyu Yesu alishinda
Aliposhuka kuzimu mbona ilinyamaza kimya Alikanyaga kifo nayo mauti ilimezwa Akatoka yu hai sasa Yesu yuko mbinguni Anatawala mbinguni anamiliki duniani Acheni huyu Yesu jamani aitwe Mungu Acheni huyu Yesu jamani aitwe Mungu mileleNimechoka kuonewa mimi namtaka Yesu
Nimechoka kuonewa, mimi namtaka Yesu Nimweleze shida zangu taabu ziniondokee Nasema sitaki, mimi namtaka YesuNamtaka Yesu nipone (Yule bwana wa mabwana)
Namtaka Yesu nipone (Yesu ni Mungu wa huruma) Namtaka Yesu nipone (yeye ni baba wa yatima) Namtaka Yesu nipone (Yesu ni mume wa wajane) Namtaka Yesu nipone (Nasema fitina sitaki) Namtaka Yesu nipone (jamani majungu sitaki) Namtaka Yesu nipone (nasema nimechoka kuonewa) Namtaka Yesu nipone (aah) Namtaka Yesu nipone (mimi majungu sitaki) Namtaka Yesu nipone (marafiki wabaya sitaki, eeh) Namtaka Yesu nipone (wenye fitina siwataki)